Thursday, October 6, 2016

Dewji awabwaga wafanyabiashara 100 vijana kwenye tuzo ya Choiseul


Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’ ametajwa kushika nafasi ya kwanza na Taasisi ya Choiseul yenye makazi yake Paris, Ufaransa kama mfanya biashara kijana ambaye anasaidia kukuza uchumi wa bara la Afrika.

MO Dewji ameshinda tuzo hiyo iliyoshirikisha wafanyabiashara vijana 100 wenye asili ya Afrika ikiwa ni mara ya tatu tangu Taasisi ya Choiseul ianze kutoa tuzo hiyo.
Choiseul imesema kuwa MO amekuwa akijihusisha kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko na kutoa nafasi kwa walio watu walio na uwezo wa kufanya kazi jambo ambalo limeleta matumaini mapya kwa Tanzania na Afrika kwa kutambua jinsi gani anawasaidia kukuza bara la Afrika na watu wake kwa kuifikisha pale ambapo wanatamani ifike.
Akizungumzia ushindi huo, MO Dewji alisema ni furaha kubwa kwake kwa kazi anayoifanya kutambulika na ataendeleza juhudi zake la kuisaidia Afrika kupata maendeleo kupitia kampuni yake ya MeTL Group.
“Ninafuraha kupokea utambuzi huu kwa ajili ya kazi ambayo nimekuwa nikifanya katika bara la Afrika. Katika safari yangu ya ujasiriamali, nitaendelea kujikita kufanya biashara, kwa kupitia MeTL, nitaendelea na dhamira yangu ya kuendeleza Afrika kupitia sekta binafsi kwa kuleta maendeleo,” alisema Dewji.

0 comments:

Post a Comment