Wednesday, October 5, 2016

Bi Samia alaani mauaji ya watafiti

Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu Hassan, amelaani mauaji ya watafiti wawili wa Seliani na dereva waliokuwa kazini katika Kijiji cha Iringa Mvumi, Chamwino.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua Kongamano ya 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumanne hii.
“Haiwezekani hata kidogo watu kufanya mauaji hayo ya kikatili na waachwe bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria,” alisisitiza Makamu wa Rais.
Bi Samia amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na watafiti hao hivyo serikali itaendelea kutoa mchango wake wa hali na mali ili kuhakikisha watafiti hao wanafanya kazi zao kwa ufanisi unaotakiwa.
Mauaji ya watafiti hao,ambao ni Teddy Nguma, Jafari Mafuru na dereva wao Nicas Magazine yalitokea Oktoba Mosi, 2016 baada ya kushambuliwa na wakazi wa kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
BY:EMMY MWAIPOPO

0 comments:

Post a Comment