Hutosikia tena kolabo kati ya msanii wa Kenya, Avril na rapper wa Bongo, Darassa, kwanini? Ngoma hiyo ipo kifungoni, walau kwa mujibu wa maneno ya Darassa mwenyewe.
Darassa akiwa kwenye studio za Wanene Entertaiment na engineer wa studio hizo (aliyekaa), Avril na producer Abbah Process
“Hiyo project na Avril, ni moja kati ya project ambazo zipo kifungoni tunasema. Hatuwezi kuirelease sababu hatutaki kuingilia taratibu za watu wala watu waingilie taratibu zetu. Project ya Avril haitatoka sababu tulirekodi kwenye studio ambayo tulikuja kutokea tafrani kidogo ya maelewano,” Darassa alimuambia Natty E wa Jembe FM.
Wimbo huo ulirekodiwa kwenye studio za Wanene Entertainment, wiki 8 zilizopita. Tafrani gani hiyo anayoisema Darassa iliyopelekea kazi yake kutiwa kifunguni? Huenda Hanscana akawa anahusika.
Wimbo huo ulirekodiwa wakati Hanscana, swahiba wa Darassa alikuwa bado mfanyakazi wa Wanene Entertainment. Baada ya muongozaji huyo kuvunja mkataba wake na kampuni hiyo, kazi zake zote alizozifanya mikononi mwao, zilipigwa kufuli – ikiwemo kazi ya mwanae Darassa!
Inasikitisha kwasababu Avril alivutiwa na kazi hiyo. “Class is in session! Really amazing getting a chance to hang out/work with @darassacmg and producer @abbah_process,” aliandika kwenye Instagram.
Darassa anabaki na option nyingine – kumleta tena Avril Bongo, kwenda kwenye studio nyingi na kumalizia walichokianza.
0 comments:
Post a Comment