Monday, October 17, 2016

Azam, Yanga, zimeshindwa kutamba uwanja wa Uhuru


Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Azam FC ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Yanga umeshuhudiwa ukimalizika bila timu hizo kufungana.
Mchezo huo ulikuwa ni wa saba kwa upande tisa kwa upande wa Azam wakati kwa Yanga ni mchezo wa nane. Yanga imeongeza idai ya michezo ambayo wametoka sare na kufikisha mechi tatu ambazo wametoka sare huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja wakati  na kushinda mechi nne Azam nao wametoka sare katika mechi tatu wamefungwa tatu na kushinda tatu.

Yanga ilipata ushindi wake wa mwisho kwenye mchezo wa Jumatano iliyopita kwa kuifunga Mtibwa Sugar goli 3-0 wakati Azam ushindi wao wa mwisho ulikuwa September 10, 2016 walipoifunga Mbeya City 2-1 uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 15 sawa na Mtibwa Sugar pamoja na Kagera Sugar lakini zikitofautiana nafasi kutokana na magoli ya kufunga na kufungwa wakati Azam wenyewe wapo nafasi ya saba kwa pointi zao 12 baada ya mechi 9

Mtukio
  • Juma Abdul alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kulazimika kupumzishwa baada ya kuumizwa na Daniel Amoah dakika za mapema kipindi cha kwanza kisha nafasi yake ikachukuliwa na Mbuyu Twite.
  • Kipindi cha pili Yanga ilipata pigo jingine kufuatia beki wake wa kati Andrew Vicent ‘Dante’ kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na mkongwe Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Matokeo
Ruvu 1-0 Mbeya City
Mtibwa Sugar 0-0 Tanzania Prisons
Toto Africans 1-2 Majimaji FC
By shaffihdauda 

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video





0 comments:

Post a Comment