Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Young Killer amesema kila kitu kipo tayari na siku yoyote atafunga ndoa.
“Kusema kweli sasa hivi tupo kwenye hatua za mwisho kabisa, yaani leo kesho mtasikia Young Killer amefunga ndoa,” alisema Young Killer. “Kwa sababu mambo muhimu yote yameshafanyika na kama vitabu vya mungu vinavyosema, mwanamke atamuacha baba yake na mama yake ataenda kwa mume wake,”
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mtafutaji’ amesema ana kila sababu ya kumuoa mpenzi wake huyo kwa kuwa ameishi naye kwa kipindi cha miaka 8.
0 comments:
Post a Comment