Mwigizaji nyota wa filamu Bongo Wastara Juma (Wastara Sajuki) leo siku ya jumatano amevikwa ubalozi wa simu zijulikanazo kwa jina la KZG Tanzania ni kampuni kutoka nchini China ikiwa pia nchini Tanzania na inapatikana nchini nzima msanii huyo aliishukru kampuni ya KZG ambao ndio wamchagua yeye kama Balozi wa simu hizo kwa mkataba wa miaka miwili mkatabata huu ameusaini mbela ya waandishi wa habari katika Hoteli ya De Mage Mwananyamala.


Tukio hilo pia liliambatana na uzinduzi wa simu ya kipekee ya KZG simu ambayo ina uwezo wa mkubwa huku ikiwa ni simu ya kwanza kuja nchini ambayo inatumia betri ndani ya simu ambalo endapo itaharibika ina uwezo wa kutengenezeka tofauti na simu nyingine ambazo zina mfumo wa aina kama hiyo na ni 4G inakaa na betri kwa muda mrefu Zaidi.
“Sisi kama KZG tumekuja kwa ajili ya kukuza teknolojia kama ilivyoanzishwa kampuni yetu pamoja na kuwa na simu pia tuna computer za KZG na tuna lengo la kuwafikia wanavyuo nchi nzima na leo hii tunamsinika ubalozi msanii wetu Wastara na tukiwa naye tutafika kila kona kutangaza bidhaa zetu,”amesema Meneja Mauzo Raymond Kalikawe.
Wastara katika sherehe hizo fupi alijumuika na wasanii wenzake kutoka Bongo Movie kama Simon Mwapagata ‘Rado’, Zuber Mohamed ‘Niva’, Daud Michael ‘Duma’, Mahsein Awadh ‘Dr. Cheni’, Deus Mihambo na kikundi cha sanaa cha Hatukwami talents group na wengine kutoka sehemu mbalimbali.







hatua nzuri hiyo
ReplyDelete