Friday, September 30, 2016

Sitarajii tena kufanya collabo na msanii wa Bongo – Dogo Janja

Rapper Dogo Janja amedai kuwa kwa sasa hana tena mpango wa kufanya collabo na msanii wa ndani ya Bongo.



Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM ya Njombe kupitia kipindi cha Supa Mega, Janjaro amedai kuwa ameshafanya collabo za kutosha na sasa ni muda wa kufanya ngoma zake mwenyewe.
Amesema anataka kuwaonesha watu kuwa anaweza kufanya muziki unaoweza kufanya vizuri bila kumshirikisha mtu yeyote ikiwemo kufanya chorus zake mwenyewe.
“Sina mpango wa kufanya collabo na msanii wa ndani,” anasema.
“Huu ni muda wangu wa kufanya kazi,” ameongeza rapper huyo anayefanya vizuri na wimbo wake Kidebe.
Hata hivyo amedai kuwa anafikiria kufanya collabo zaidi za kimataifa. Msikilize zaidi hapo chini.

0 comments:

Post a Comment