Saturday, September 24, 2016

Movie ya Fast and Furious 8 itakayotoka 2017, Justin Bieber ndani


Najua kuna watu wangu ni wapenzi wa movie na wasanii wa nje, Good news! kwenu imeripotiwa leo na kituo cha habari E daily news kuwa movie ambayo wote mmekuwa mkiisubiria kwa hamu Fast and Furious 8 itakayozinduliwa mwanzoni mwa 2017kunauwezekano msanii kutoka CanadaJustin Bieber kuigiza pia.
Kumekuwa na taarifa pia kutoka, Movie Pilot kwamba Justin Bieber ataungana na waigizaji wa movie hiyo katika season nyingine tena ya 8, na pia Msanii huyo amekuwa akifahamiana sana na Director wa Movie hiyo anayeitwa Gary Gray .

Iliendelea kuelezwa kuwa Justin alitaka kushutiwa kwenye movie hiyo tangu 2012 ambayo ilikuwa Fast and Furious 7 lakini haikuwezekana kutokana sababu kwamba hakuwa amefanya mazoezi ya kutosha na akashauriwa kuendelea na mazoezi kwanza.
Ilipofika 2013 alipofariki mmoja wa waigizaji wa movie hiyo Paul Walker  ikasemekana Justin kuziba pengo lakini haikuwa hivyo likazibwa na Cody Walker, zaidi wametaja kuwa Justin sasahivi amejiandaa kikamilifu na inasemekana kuigiza kwenye movie ya msimu huo wa 8.

0 comments:

Post a Comment