Showing posts with label By jcb. Show all posts
Showing posts with label By jcb. Show all posts

Thursday, October 6, 2016

BENKI YA DUNIA YAITAHADHARISHA TZ


The International Bank for Reconstruction and Development -IBRD (BENKI YA DUNIA), katika ripoti yake mpya imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 katika Bara la Afrika ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi, lakini imeonya kuwa kunahitajika juhudi za makusudi katika kuhakikisha kuwa ukuaji huo uzingatie mgawanyo wa kinachopatikana wenye kuleta ustawi na kupunguza kiwango cha utofauti wa matajiri na maskini.
Katika Taarifa yake hiyo, Benki ya Dunia imeitaka Tanzania kuwa na msukumo mpya katika kukabiliana na hali ya kutokuwa na usawa wa kiuchumi pamoja na Takwimu za miaka kumi mfululizo kuonesha zipo juu, bado hali ya wananchi haijakombolewa kutoka kwenye lindi kubwa la umaskini.

Read More

Monday, September 26, 2016

FORBES WASIFU NDEGE MPYA ZA JPM



JARIDA mashuhuri duniani la Forbes, limezitaja ndege aina ya Bombardier Dash8 Q400, ambazo tayari Tanzania imezinunua kuwa ni zenye usalama, zinazotumia mafuta kidogo. Limetabiri kuwa zitakuwa nguzo muhimu kwa usafiri wa bei nafuu kwa nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa na jarida hilo ikiwa na kichwa cha habari “Can Bombardier’s Q400 Save Regional Air Service in the US?”, mwandishi anafafanua faida ya ndege hizo, ikilinganishwa na ndege nyingine zinazofanya usafiri wa ndani nchini Marekani.



“Bombadier ina kasi nzuri na ya kutosheleza mahitaji ya safari za ndani kwa kiwango cha kuwa na faida zaidi kibiashara, ikilinganishwa na ndege nyingine za aina yake kama ATR,” linaandika jarida hilo la Forbes.

Aidha, jarida hilo linataja faida nyingine ya ndege hizo kuwa ni uwezo wa kutumia mafuta kidogo, jambo litakalosaidia kupunguza gharama za usafiri huo wa ndege nchini kwa wasafiri wa ndani. Jarida hilo linafafanua kuwa kiwango kidogo cha mafuta, kinachotumiwa na ndege hizo, kunazifanya kuwa na ufanisi wa asilimia kati ya 48 mpaka 50 zaidi ya ndege nyingine.

Forbes linasisitiza kuwa kutokana na gharama za matengenezo kupanda na gharama nyingine za uendeshaji, ikiwemo mishahara mizuri kwa marubani, kuna uwezekano mkubwa kwa Bombardier kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza tiketi kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege nyingine.

“Kwa sasa tunakadiria kuwa ndege aina ya Bombardier, ndizo zitakuwa mbadala na zitashika njia nyingi za ndani (Marekani) kwa kiasi cha asilimia 50 hadi 60 na zitasaidia kurejesha usafiri uliositishwa kutokana na gharama kubwa kwa ndege nyingine katika viwanja takribani 20,” linafafanua jarida hilo.

Sunday, September 25, 2016

JELA MAISHA KWA KUCHOMA MOTO MAKANISA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoani Kagera imewahukumu kifungo cha maisha watu watatu kwa makosa ya kula njama na kuchoma makanisa mbalimbali mkoani hapa.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Emmanuel Manyere alisema licha ya hukumu hiyo, bado watu hao watatu wanakabiliwa na kesi ya kukata makoromeo na mauaji ya watu 16 ambayo inaendelea katika Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba.

Manyere alisema watu hao watatu ambao ni Allyu Dauda, Rashid Mzee na Ngesela Keya walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, mbele ya Hakimu Mkazi wa Bukoba, Victor Biambo.

Alisema washtakiwa hao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya kula njama na kuchoma makanisa 16 ya madhehebu mbalimbali mkoani hapa.

Hakimu Bigambo alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi kutoka upande wa walalamikaji na kutoa adhabu ya kifungo cha miaka saba jela kwa wote watatu kwa kosa la kula njama na kifungo cha maisha kwa kosa la kuchoma makanisa.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Augustino Ollomi aliipongeza Mahakama kwa kutenda haki katika kesi hiyo pamoja na kuwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa polisi ili kukomesha vitendo kama hivyo.