Friday, September 1, 2017

Mahakama Kuu imebatilisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu Kenya

Mahakama Kuu Kenya imebatilisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika August 8, 2017 ambao ulimpa ushindi Uhuru Kenyatta dhidi ya Raila Odinga na kutaka kuandaliwa uchaguzi mwingine ndani ya siku 60.

Mahakama hiyo imeeleza kuwa IEBC haikuandaa uchaguzi huru na wa haki ambapo Jaji Mkuu David Maragaameagiza uchaguzi haukuandaliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria, hivyo matokeo yake ni batili.
“Natangaza hapa kwamba Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa. Agizo linatolewa, kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha Uchaguzi mwingine kwa kufuata Katiba na Sheria katika kipindi cha siku 60.” – Jaji Maraga.
Hatua hiyo imekuja baada ya mgombea Urais kupitia Muungano wa Upinzani NASA, Raila Odinga kufungua kesi Mahakamani kupinga matokeo yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta ambaye alitangazwa mshindi na Tume Huru ya Uchaguzi IEBC.
Kesi hiyo ilikuwa na Majaji Saba ambao wawili kati yao; Justice Jackton Ojwang’ na Njoki Ndung’u walisema Uchaguzi huo uliendeshwa kwa misingi ya haki na huru.
Kwa uamuzi huo sasa Uhuru Kenyatta hatoapishwa kama Rais Mteule bali atasubiri tena matokeo baada ya Uchaguzi utakaoitishwa ndani ya siku 60.


source:Mtandao
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment