Thursday, July 27, 2017

Lissu apata dhamana

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania, Mhe. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 leo katika kesi yake iliyokuwa inamkabili ya uchochezi.
Mahakama ya Kisutu imempa dhamana Mh Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya thamani ya milioni kumi.
Uamuzi huo umetolewa mbele ya mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri. huku kwa upande wake Lissu alikuwa anatetewa na jopo la mawakali 18 likiongozwa na Fatma Karume na Peter Kibatala ambapo katika shauri la kwanza waliomba Mahakama impe dhamana mteja wao.
Kwa upande mwingine, Lissu alitiwa katika mikono ya dola mnamo Julai 20 siku ya Alhamsi katika uwanja wa ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. na siku iliyofuata  jeshi hilo lilikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Mbunge huyo.


Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment