Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo aliyefariki dunia atazikwa Jumanne ijayo Mbokomu Mashi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema kuwa Ndesamburo atazikwa katika makaburi ya familia nyumbani kwake eneo la Mbokomu.
Golugwa amesema Jumatatu, kwenye viwanja vya mashujaa mjini Moshi wananchi watapata fursa ya kuaga mwili wa Ndesamburo. Katibu huyo amesema wakati wa kuaga mwili wake kutakuwa na salamu kutoka kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini na wawakilishi wa makundi mbalimbali.
Golugwa amesema msiba wa Ndesamburo umewagusa wengi nchini kutokana na mchango wake katika kukuza misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuchangia ustawi wa sekta ya utalii.
Na Emmy Mwaipopo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment