Thursday, May 18, 2017

Waziri Mwigulu- Majeruhi kutibiwa bila PF3

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka, na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata apewe matibabu bila fomu ya PF3.
Kwa mujibu wa agizo la Waziri Mwigulu amesema hatua za kupata fomu ya matibabu PF3 kutoka polisi ziendelee wakati mgonjwa akiendelea kupata matibabu na lengo likiwa ni kuokoa maisha yao kwanza.
Mwigulu ameongeza  "Utaratibu huo utakuwa ukifatiliwa kwa karibu kutoka kwenye vyombo vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la muhusika" Waziri Mwigulu Nchemba

Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment