Monday, May 8, 2017

Samatta kafunga na kuisaidia Genk kupata ushindi

Usiku wa Mei 7, 2017 mshambuliaji Mbwana Samatta aliifungia timu yake ya Genk goli moja na kuisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya AS Eupen katika mechi ya play off ya ligi ya Ubelgiji.
Samatta ali-assist goli la kwanza lililofungwa na Jere Uronen dakika ya 18 kipindi cha kwanza. Samatta alipiga shuti kali ambalo lilimgonga beki kisha kumkuta Uronen ambaye aliukwamisha mpira kambani.
Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta akafunga bao la pili dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri iliyifanywa na Thomas Buffel na kuipa Genk uongozi wa 2-0.
Eupen walipata goli lao pekee dakika ya 76 kupitia kwa H.C. Onyekuru na kupelekea mchezo kumalizika kwa Genk kuibuka washindi wa mchezo kwa magoli 2-1.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment