Wednesday, May 24, 2017

Ni United vs Ajax leo, lakini wajua Ajax hawajawahi kupata hata suluhu kwa Mourinho?

Leo ni leo katika dimba la Friends Arena nchini Sweden, uwanja ambao hauna bahati ya fainali lakini leo umebahatika kwa fainali kati ya Manchester United na Ajax ya Uholanzi.
Ushindi wa Manchester United leo utawapa tiketi kucheza champions league msimu ujao lakini wakifungwa watacheza tena Europa, wakati macho yote yakielekezwa Friends Arena sii vibaya ukajua mambo muhimu kuelekea mchezo huo.
Ajax inakuwa timu ya kwanza kutoka nchini Uholanzi kufika fainali ya michuano hiyo ya Europa tangia mwaka 2002 ambapo Feynoord walifanya hivyo
Katika misimu mitano ya ligi kuu Uingereza Manchester United inakuwa timu ya 3 kufika fainali hiyo baada ya Liverpool(2016) na Chelsea (2013).
Manchester United na Ajax wameshakutana mara 4 katika michuano ya barani Ulaya lakini hakuna mbabe, kwani kila mmoja amemfunga mwenzie mara mbilimbili wakati walipokutana.
Hii ni fainali ya kwanza ya Ajax katika michuano ya Ulaya baada ya ile ya mwaka 1995 dhidi ya Juventus katika champions league ambapo Ajax alifungwa kwa mikwaju ya penati.
Manchester United wanaingia katika mchezo huu kifua mbele kwani hadi wanafika fainali hawajawahi kupoteza mchezo katika michezo 10 iliyopita, wakisuluhu mara 3 na kushinda mara 7.
Jose Mourinho ni mbabe haswa wa Ajax, hadi sasa Mourinho ameshakutana na Ajax mara 6 na katika mara zote hizo walichezea kichapo kutoka kwa Mreno huyo.
Kasper Dolberg wa Ajax ana mabao 6 hadi sasa na ni Patrick Kluivert na Tin Blanker tu ambao walifunga mabao mengi kuliko yeye katika michuano ya Ulaya, walikuwa na mabao 7.
Katika fainali 16 zilizopita za Europa ni fainali 2 zilamuliwa kwa mikwaju ya penati, fainali 10 ziliamuliwa kwa muda wa nyongeza na huku fainali 4 zikiamuliwa muda wa kawaida.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment