Taarifa zilizonifikia kutoka Hospitali ya Muhimbili zinasema mzee Francis Kanyasu maarufu kama Ngosha, ambaye amehusika kwenye kuchora Nembo ya Taifa Tanzania, amefariki dunia akiwa kwenye matibabu hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa taarifa inaelezwa kuwa May 29, 2017 hali ya mzee huyo ilibadilika ghafla na madaktari walijitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kunusuru maisha yake lakini ilishindikana na akafariki duniani saa 2 usiku.
Mwili wa mzee huyo upo chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo ambapo unasubiri mamlaka husika kutoa maelekezo zaidi.
source:millardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment