Jana kulikuwa na mchezo kati ya Manchester United waliokuwa ugenini kuikabili Tottenham ambapo mchezo huo umemalizika kwa United kuchezea kichapo cha mabao mawili kwa moja.
Baada ya mchezo huo kama kawaida waandishi wa habari huwa wanafanya mazungumzo na makocha wa timu zote mbili ili kujua wanauzungumziaje mchezo huo.
Wakati mtangazaji mmoja akimuuliza Mourinho juu ya kipigo kutoka kwa Tottenham, Mourinho alimjibu mtangazaji huyo kwamba huo ulikuwa mchezo ambao hawakutaka kuucheza.
Mourinho kwa sasa ameelekeza akili yake yote katika mchezo wa fainali ya mashindano ya Europa dhidi ya Ajax baada ya kuona ni ngumu kwa wao kumaliza ligi katika nafasi nne za juu.
Mourinho ambaye anakabiliwa na mejuruhi wa mara kwa mara katika timu yake amesema ni ngumu kushiriki michuano mikubwa miwili ukiwa na idadi chache ya wachezaji na ndio maana anaowashangaa wanaoongea kuhusu United kuiwaza zaidi Europa.
Pamoja na kipigo hicho toka kwa Tottenham Mourinho hakusita kutoa sifa kwa wachezaji wake huku akisema ukiangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja hakika walijitahidi sana uwanjani.
Wakati mtangazaji wa shirika hilo lililokuwa likimfanyia mahojiano Mourinho akijiandaa kuuliza swali la nne, kocha huyo wa Manchester United aliamua kuondoka zake.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment