Rapper Profesa Jay amedai kuwa amewasamehe wasanii wenzake ambao walitaka akose ubunge.
Jay ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi, kupitia mtandao wa Instagram amewataka wasanii wawe na umoja. Kupitia mtandao huo ameweka kile kinachoonekana ni mashairi ya wimbo wake mpya Kibabe (The Icon):
Nilishawasamehe Wasanii wenzangu,
Waliokuja jimboni kupinga Ubunge wangu,
Mabasi na Mabasi Jiongezeni wanangu,
Asante wana MIKUMI kwa kuwa na Imani kwangu #KIBABE (The ICON )#Sanaa yataka umoja nitakubeba UKIANGUKA.
0 comments:
Post a Comment