Friday, March 17, 2017

HANS VAN PLUIJM ATUA RASMI SINGIDA UNITED

Klabu ya Singida United iliyopanda daraja kuingia ligi kuu msimu ujao, imethibitisha kuingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha na Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Hans Van Pluijm.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Abdulrahaman Salum Sima, imesema kuwa makubaliano na kocha huyo wa Kimataifa wa Uholanzi yamefikiwa leo Ijumaa tarehe 17, Machi, 2017 lengo likiwa ni kukata kiu ya mafanikio ya klabu hiyo.
Amesema mbali na kocha huyo, klabu hiyo pia imeingia makubaliano na kinda wa kimataifa Tafadwaza Kutinyu ambaye anacheza katika nafasi ya kiungo kutoka timu ya Chicken inayoshiriki Ligi Kuu ya Zimbabwe.
“Ni moja ya malengo makubwa ya klabu yetu kuona inasajili Kocha, wachezaji wazuri wenye sifa za kucheza michuano yote ya ndani na nje ya nchi yetu. Hivyo Kocha Hans ni hatua kubwa kwetu na tuna imani kuwa hii itaisogeza Singida United kwenye ramani ya soka barani Afrika na baadaye duniani kote” Amesema Katibu Mkuu Sima


Source:perfect255
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment