Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Kiungo wa Timu ya Taifa ya Uingereza Frank Lampard ametangaza rasmi kutandika Daluga na kusalia kuwa mtazamaji na kuchukua mafunzo ya Ukocha.
“Baada ya miaka 21 ya ajabu, Nimeamua kwamba sasa ni wakati muafaka wa kumaliza kazi yangu kama mchezaji wa kitaalamu. Wakati nimepokea idadi ya ofa za kusisimua ili kuendelea kucheza soka la nyumbani na nje ya nchi, katika umri huu wa miaka 38 Naona sasa ni wakati wa kuanza sura ya pili katika maisha yangu.
“Naona fahari, kwa kuwa nimekuwa mshindi, ambae ninayewakilisha nchi yangu zaidi ya mara 100 na kwa mabao zaidi ya 300, hiyo yote nikufanya kazi kwa malengo. Sehemu kubwa ya moyo wangu ni mali ya Chelsea, klabu ambayo imenipa kumbukumbu nyingi kubwa ,”alisema. “Mimi kamwe siwezi kusahaunafasi ambayo wao walinipa na mafanikio ambayo sisi tumeweza kufikia pamoja.
Aliendelea, “Haiwezekani kutoa shukrani kwa mmoja mmoja kwa watu wote ambao walisaidiana na mimi katika miaka yangu 13 kwa kucheza huko. Ninachoweza kusema ni kuwa tokea siku mimi nasaini hadi sasa na kwenda mbele, na kushukuru milele kwa kila kitu na kwa kila mtu . Mashabiki wa chelsea pamoja na wachezaji wenzangu walinionesha ushirikiano wa ajabu. upendo wao umenifanya kuwa hivi nilivyo leo hii. Nisingeweza kuwa hivi leo bila wao.“
Alimalizia, “Natarajia kutafuta fursa nyingine nje ya uwanja, ambapo naamini uamuzi huu utasaidia“
Frank Lampard amenyakua mataji matatu ya EPL, Makombe manne ya FA, vikombe viwili vya kombe la Ligi, Taji moja la Klabu Bingwa Ulaya na Europa, na kumfanya atimize michezo 1039 na Magoli 302 kwa miaka 21 aliyoitumikia kama mchezaji kwenye vilabu mbalimbali na Timu yake ya Taifa.
0 comments:
Post a Comment