Wednesday, February 1, 2017

Chelsea na Liverpool walilazimishana sare ya 1-1 na msimamo wa EPL ulivyo

Usiku wa January 31 Liverpool waliwakaribisha Chelsea katika uwanja wao wa Anfield kucheza mchezo woa wa 23 wa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017, Liverpool waliingia katika mchezo huo staa wao Saido Mane akiwa kaanzia katika benchi.
Sadio Mane alikuwa benchi katika mchezo huo uliyomalizika kwa sare ya 1-1 kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia 100, hivyo alikuwa benchi akiwa kawekewa barafu lakini aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho.
Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli dakika 25 kupitia kwa David Luiz aliyefunga goli hilo kwa mpira wa adhabu, ila Liverpool walisawazisha goli hilo dakika ya 58 kupitia kwa Georginio Wijnaldum na kuufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya 1-1.
Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya mechi za January 31 2017


View image on Twitter

0 comments:

Post a Comment