Tuesday, January 17, 2017

WANAWAKE KENYA WAJIFUNZA KARATE KUPAMBANA NA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Vitendo vya unyanyasaji wa kijinsi ambavyo vinajitokeaza katika maeneo mbalimbali nchini Kenya vimewashawishi wanawake wa eneo la Korogocho lililopo Nairobi Kenya kutafuta njia mbadala ya kuzuia vitendo hivyo.
Wazee wa jinsia kike katika eneo hilo wameunda kikundi ambacho kitakuwa kikifanya mazoezi ya pamoja ya karate ili kuweka miili yao fiti ili hata wanaume wanapowafata kwa lengo la kuwaingilia kimwili bila ridhaa yao waweze kuwadhibiti.
Akielezea hali ilivyokuwa awali kabla ya kuweka kikundi hicho, Beatrice Nyariara alisema kwa kipindi kirefu wanawake wa eneo hilo wamekuwa wakinyanyaswa na wanaume na hasa vijana lakini sasa mambo ni tofauti tangu walipoanzisha kikundi.
“Hali sio salama sababu kabla hatujaanzisha kikundi kwa wazee kama mimi, wanawake wengi wazee walikuwa wakibakwa na vijana wadogo. Wanatumia madawa ya kulevya, pombe na wakirudi nyumbani hawajui kutofautisha wazee na mabinti wa kike,” alisema Beatrice.


Source:dewjiblog
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video



0 comments:

Post a Comment