Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Brennan amemuonya Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump kuwa makini na kauli zake na kuuchunga mdomo wake, hasa anapozungumzia suala la uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Urusi kwa madai kwamba anahatarisha usalama wa Taifa la Marekani.
Brennan aliendelea kueleza kuwa, Trump bado hajaelewa nia ya Urusi kwa Marekani kwa hiyo badala ya kufurahia mipango ya siri inayoendelea, anapaswa kuwa makini na kuchunga kauli zake.
“Nafikiri Trump haelewi kwa sababu gani uhusiano wa Marekani na Urusi umekuwa suala tete kwa kipindi kirefu kilichopita, anatakiwa kuwa makini sana anapolishughulikia suala hili,” alisema na kuongeza kuwa CIA inazo taarifa za namna Urusi inavyojaribu kumtumia Trump kutimiza matakwa yake.
John Brennan
Brennan aliyazungumza hayo wakati akihojiwa na Kituo cha Runinga cha Fox News, ikiwa ni wiki moja tangu alipotangaza ripoti kwamba wamegundua kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin na vijana wake, walifanya ‘makeke’ ili Trump ashinde kwenye uchaguzi mkuu nchini humo, na kumuangusha kwa hila mpinzani wake, Hillary Clinton.
0 comments:
Post a Comment