Tuesday, January 31, 2017

Aliyekuwa kocha wa Taifa Star, Boniface Mkwasa atangazwa rasmi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa Jumanne hii ametangazwa rasmi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga.
Mkwasa mwenye taaluma ya ukocha daraja la kwanza la CAF, amewahi kuzifundisha klabu mbalimbali ikiwemo Yanga kwa vipindi tofauti na timu za taifa za wanaume na wanawake.
Kabla ya hapo, Mkwasa alikuwa kocha wa timu ya Taifa Stars kwa kipindi cha miezi 17 kabla ya TFF kusitisha mkataba wake mapema Januari 2017.
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amemtambulisha Mkwasa leo mbele ya waandishi wa habari na kusema kocha huyo ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, ameingia mkataba wa miaka miwili.
Mkwasa anachukua nafasi ya Baraka Deusdedit aliyekaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, kufuatia kuondoka kwa Jonas Tiboroha mapema mwanzoni mwa mwaka jana.
“Kwa niaba ya uongozi mzima wa Yanga Sc namtangaza rasmi sasa Boniface Mkwasa mchezaji wetu na mwalimu wetu wazamani kuwa ndie katibu mkuu mpya wa klabu yetu ya Yanga Sc”



0 comments:

Post a Comment