Monday, December 12, 2016

Man United imepata ushindi wa kwanza Old Trafford tangu September

Goli pekee la Henrikh Mkhitaryan limeipa Manchester United ushindi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Old Trafford katika michezo ya Premier League, mara ya mwisho Man United kuibuka na ushindi O.T ilikuwa ni mwezi September.
United bado wako nyuma kwa pointi sita dhidi ya Manchester City ambayo ipo ndani ya top four.
Rekodi nne zilizowekwa baada ya mchezo wa Manchester United vs Tottenham
  • Manchester United imepata ushindi wa kwanza ndani ya Premier League kwenye uwanja wa Old Trafford tangu mwezi September, imetoka sare katika mechi zake nne mfululizo zilizopita kwenye uwanja wao wa nyumbani.
  • Kwa mara ya kwanza Tottenham imepoteza mechi mbili mfululizo za ugenini tangu iwe chini ya Mauricio Pochettino, mara ya mwisho ilikuwa ni March 2014 (walipoteza mechi tatu).
  • Spurs hawajashinda mechi zao tano za ugenini ndani ya Premier League, ni kipindi kirefu zaidin tangu mwaka 2012 (walicheza mechi 8 ugenini bila kushinda).
  • Henrikh Mkhitaryan amehusika katika magoli manne katika mechi nne za mwisho alizoichezea Manchester United (amefunga magoli mawili na ku-assist mara mbili).


Source:shaffihdauda
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video



0 comments:

Post a Comment