Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Algeria Georges Leekens ameitahadharisha Nigeria kuwa iwe makini katika mchezo wao wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018, kwani wanakwenda kucheza na timu bora barani Afrika.
Leekens ameteuliwa siku 16 kabla ya mchezo huo utakaopigwa Novemba 12 mjini Uyo Nigeria, akichukua mikoba ya Milovan Rajevac aliyetimuliwa kazi.
Akiongea mbele ya wanahabari kwa mara ya kwanza Leekens amesema anaelewa changamoto inayomkabili kuwania kufuzu kombe la dunia lakini hiyo haimpi taabu kwani hata wapinzani wao wanajua wanakwenda kucheza na timu bora Afrika.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo (Faf) Mohamed Raouraoua Leekens raia wa Ubeligji na Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ubeligji tayari ameshataja kikosi akimjumuisha nyota wa Leicester City Riyard Mahrez.
Source:mtembezi
0 comments:
Post a Comment