Thursday, November 24, 2016

MWINYI AKUNWA NA JITIHADA ZA JPM ZA KUNYOOSHA NCHI

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema Rais John Magufuli ameleta tsunami kwa wabadhirifu wa fedha za umma kupitia falsafa yake ya kutumbua majipu.

Aliyasema hayo jana wakati alipokutana na Rais Magufuli na kufanya naye mazungumzo, Ikulu Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kiongozi huyo aingie madarakani mwaka mmoja sasa.

Kupitia falsafa yake ya kutumbua majipu, Dk Magufuli amechukua hatua za kuwasimamisha na kuwafuta kazi baadhi ya watumishi wa umma wakiwemo wakurugenzi wa taasisi nyeti.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana ilifafanua kuwa baada ya mazungumzo hayo, Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa alisema lengo la kukutana na Rais Magufuli na kufanya naye mazungumzo ni kumpongeza kwa kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani na pia kumpongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Mwinyi aliyataja baadhi ya maeneo ambayo Rais Magufuli ameyafanya kwa mafanikio makubwa kuwa ni mapambano dhidi ya rushwa na akabainisha kuwa hatua zilizochukuliwa katika kipindi cha mwaka mmoja zimedhihirisha kasi kubwa ya kukabiliana na tatizo hilo ikilinganishwa na wakati uliopita.

“Rushwa ilikuwepo tangu enzi ya Mwalimu Nyerere, aliipondaponda kabisa lakini hakuimaliza, na sote tuliosalia ni hivyo hivyo, kila mmoja amefanya kwa kiasi chake, lakini Rais Magufuli kwa mwaka mmoja ameleta tsunami, nafurahi sana,” alisema Mzee Mwinyi.



Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video








0 comments:

Post a Comment