Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya siku 10 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu papo kwa hapo, leo ni zamu ya Temeke baada ya kuhitimisha ziara yake katika wilaya ya Kigamboni.
Akiwa katika ziara yake ya DARMPYA katika wilaya ya Temeke RC Makonda amefanya mazungumzo na watumishi wa Halmashauri ya Temeke na kuwaomba watumishi hao wafanye kazi kikamilifu kwa mujibu wa majukumu yao ili kupunguza matatizo mbalimbali yanayo wakabili wananchi, na kueleza kuwa serikali inawatumishi wengi na mambo yamekuwa hayaendi sawa ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo kufanywa chini ya kiwango.
Hivyo RC Makonda ameeleza kuwa kufuatia kutokuwajibika kwa watumishi wa umma anampango wa kumshawishi Rais Magufuli waanze kuwapunguza watumishi wasiofanya kazi kwa maslahi ya umma, huku akisisitiza kuwa serikali ya Rais Magufuli inahitaji kuona matokeo ya kazi ya mtumishi wa umma na sio amekaa muda gani kwenye kazi.
Katika hatua nyingine RC Makonda amewataka watumishi wa umma kujiongeza na kutotegemea bajeti ili kukamilisha miradi ya maendeleo huku akitolea mfano kuwa kwa kipindi alichokaa madarakani amepokea zaidi ya bilioni 30 nje ya bajeti, hivyo ni vyema na wao wakaiga mfano huo.
Source:mtembezi
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
0 comments:
Post a Comment