Baada ya Taarifa kuwafikia waandaji wa tuzo kuwa walikosea katika kugawa tuzo hiyo ambayo ilistahiki kuja Bongo kwa Alikiba, Sasa msanii kutoka Nigeria Wizkid imeonekana kama amechukizwa na jambo hilo na kuamua kufuta picha zake zote za tuzo za MTV.
Hii ni moja ya picha ambayo aliiposti Wizkid katika kurasa yake ya Instagram baada ya kushinda tuzo za MTV MAMA
Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri katika akaunti ya Instagram ya Wizkid utagundua kuwa baadhi ya picha ambazo Wizkid alikuwa ameshinda tuzo za MTV amezifuta zote na hii inasemekana kuwa ni baada ya MTV EMA kufanya makosa katika ugawaji wa tuzo hiyo.
Source:perfect255
0 comments:
Post a Comment