Thursday, October 27, 2016

Waziri Mbarawa ameitaka bodi mpya ya Shirika la Posta kusimamia mapato


Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi  teule ya Shirika la Posta kutumia fursa zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika hilo.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Jijini Dar es Salaam.
“Nashukuru kwa kuwa mmekubali uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafuta mapato na shirika hili la Posta lina vyanzo vingi  lakini bado halijatumika vizuri na hivyo naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele” Alisema Prof Mbarawa.
1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Aidha Waziri Mbarawa ameitaka bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata matokeo mazuri  na amesisitiza kuboreshwa kwa mahusiano kati ya watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.
Waziri Mbarawa ameagiza bodi iyo teule  kusimamia huduma mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa uadilifu ili vilete tija kama ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo kuwa serikali imejipanga  kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza mzigo wa utendaji wa shirika hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Mstaafu Haruni Kondo amemhakikishia waziri huyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya Shirika hilo  na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinapatikana kama alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa maendeleo wa shirika hilo.
Na Daudi Manongi, MAELEZO
4Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
2Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora akisoma taarifa ya utekelezaji wa Shirika la Posta kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa  Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo uliofanyika jijini Dar es salaam.
3Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Dkt. Haruni Kondo akisoma taarifa ya uendeshaji wa Shirika hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
5Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kwenye begi lilobeba vitendea kazi vya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora.
6Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)




Source: dewjiblog

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video



0 comments:

Post a Comment