Kim Kardashian amepata mshirika wa kumsaidia kuwawinda majambazi waliomvamia na kumshikilia kwa mtutu wa bunduki Jumatatu hii na kumuibia mali za thamani kubwa.
Si mwingine, bali ni Rais wa Ufaransa, François Hollande.
Watu waliokaribu na staa huyo, wanadai kuwa baada ya tukio hilo la Paris, Hollande yeye mwenyewe anahusika katika uchunguzi na ameahidi kutoa ulinzi wa ziada kwa Kim mara nyingine akiwa nchini humo, kwa mujibu wa Pagesix.
Kutokana na tukio hilo kuteka habari za wiki hii dunia, mamlaka za Ufaransa zitaabika iwapo zitashindwa kuwakamata watu hao watano waliokuwa wamefunika sura zao na Hollande anataka watu maarufu akiwemo Kardashian, kurejea na kujihisi wako salama Paris.
Wakati huo huo, kuna taarifa kuwa anatafutwa mtu anayefanana na Kim ili kumtumia kuchanganya watu na kumhakikisha usalama zaidi kila anapotoka nje.
Pia watoto wake, North na Saint, watakuwa na timu yao ya ulinzi kwakuwa Kim ana wasiwasi kuwa wao pia wanaweza kutekwa. Kutokana na tukio hilo Kanye anadaiwa kumuonya mke wake kutomuamini mtu yeyote ndani ya timu yake.
0 comments:
Post a Comment