Monday, October 17, 2016

Pogba ajitetea, asema anahitaji muda kuzoea ligi ya Uingereza


Mchezaji wa Manchester United ambaye pia ndiyo mchezaji ghali zaidi kwa sasa duniani, Paul Pogba amezungumza kuhusu uwezo wa soka ambao amekuwa akionyesha uwanjani kutokana na kuwa akitupiwa lawama kuwa kiwango chake kimeshuka.
Pogba alisema kumekuwa na watu wakosoaji ambao wamekuwa wakimzungumzia uwezo wake lakini yeye hajali na anadhani anahitaji muda ili kuzoea timu anayoitumikia ya Manchester United.
“Nahitaji muda kidogo kuizoea Manchester, muda ambao mashine itaanza kufanya kazi nitakuwa nimezoea,” alisema Pogba wakati akizungumza na French TV na kuongeza.
“Watu wanapenda kuzungumza kuhusu Pogba, ni wakosoaji kila siku, ila mimi sijali, naweka muziki na kucheza”
By dewjiblog 

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 


0 comments:

Post a Comment