Thursday, October 6, 2016

Mtoboa Macho alishinda milioni 20 za Dume Challenge, mshiriki mwenzake amwelezea alivyomfahamu

Wiki hii, habari kubwa nchini ilikuwa ni tukio la mfanyabiashara, Said Ally kutobolewa macho,  usiku katika maeneo ya Buguruni Sheli jijini Dar es Salaam.

scorpion baada ya kukamatwa na kupandishwa kizimbani

Jina la ‘Scorpion’ – mtu aliyefanya unyama huo, limekuwa maarufu pia. Polisi tayari wamemkamata na Jumatano hii alipandishwa kizimbani kusomewa mashtaka mbalimbali yakiwemo kupora na kumjeruhi Said kwa kumchoma visu mwilini na kumtoboa macho yake na kumpa upofu wa ukubwani.
SCORPION NI NANI?

Jina lake halisi ni Salim H Njwete au Samjet. Unaweza ukawa umewahi kumuona sehemu. Mwaka 2012, alikuwa mshindi wa shindano la Dume Challenge lililowakutanisha vijana 20 wababe wa mazoezi na kazi ngumu. Salim alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 20.
Read More..........

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 

0 comments:

Post a Comment