Sakata la posho za madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha halijapoa, baada ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) kuliibulia kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac), akisema linakwamisha ukusanyaji wa mapato.
Selasini aliibua suala hilo jana wakati kamati ilipopitia na kuhoji hesabu za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Alisema halmashauri hiyo imekata posho kwa madiwani na watendaji na kuzipeleka fedha kwa walimu, jambo ambalo linawavunja moyo wawakilishi hao wa wananchi kutimiza majukumu yao.
Source: mtembezi
0 comments:
Post a Comment