Mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, rais mstaafu Jakaya Kikwete amekitaka chuo kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) kilinde hadhi yake ya kuendelea kuwa kiongozi katika utoaji wa elimu bora.
Source: bongo5
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho, Kikwete alisema hatua ya chuo hicho kufikisha umri huo ni wazi kuwa kimekomaa na kimetoka katika hatua mojawapo ya makuzi na kwenda nyingine, hivyo kinastahili kuwa chachu ya maendeleo kwa kutoa wahitimu wenye kuleta mabadiliko katika nchi.
“Nawasihi mafanikio ambayo mmeyapata kwa miaka 55, endeleeni kuwa kitovu cha kutoa elimu bora. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiongoze wengine wafuate,” alisema.
Aidha Kikwete ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa mkuu wa chuo hicho, alisema licha ya chuo hicho kutoa mchango mkubwa kwa nchi ikiwa ni pamoja na kutoa viongozi wa nchi na wataalamu ambao wamekuwa msaada mkubwa katika kutunga sera za nchi, kinatakiwa kutoa wahitimu ambao wanakidhi soko la ajira.
Rais Mstaafu huyo ni miongoni mwa wanafunzi waliosoma katika chuo hicho. Alikuwa mwanachuo katika miaka ya 1975.
BY: EMMY MWAIPOPO
Source: bongo5
0 comments:
Post a Comment