Shirikisho la soka nchini TFF limemtangaza mshambuliaji wa klabu ya Simba Shiza Kichuya kuwa mchezaji bora wa mwezi September baada ya jopo la wataalamu kuchambua kwa kina na kuona mchezaji huyo amekidhi vigezo vya kuwa mshindi wa tuzo hiyo akiwabwaga wachezaji wengine wawili.
Alfred Lucas amemtangaza Kichuya kushinda tuzo hiyo akifuata nyayo za John Boco aliyeshinda tuzo hiyo kwa mwezi August.
“Mshambuliaji wa Simba Shiza Ramadhani Kuchua amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi September.”
“Kichuya amewashinda washambuliaji Adam Kingwande wa Stand United na Omary Mponda wa Ndanda FC.”
“Kichuya aliisaidia klabu yake ya Simba katika mwezi September kupata pointi 12 katika mechi nne ambazo ilicheza matokeo ambayo yameifanya Simba kuendelea kuongoza ligi.”
“Alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne alizocheza. kwa kushinda tuzo hiyo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni moja kutoka kwa mdhammini wa ligi kuu Tanzania bara.”
0 comments:
Post a Comment