RAIS John Magufuli amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuwa taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amemuengua ukuu wa mkoa wa Arusha, sio za kweli, kwani ni uzushi unaopaswa kupuuzwa.
Hayo yalisemwa na Gambo, wakati akitoa maelezo ya mwisho katika kikao cha wafanyabiashara wakubwa wa mkoani Arusha, aliokutana nao kusikiliza changamoto, zinazowakabili na kuzifanyia kazi ili waweze kufanya kazi bila wasiwasi.
Gambo aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa Rais amempigia simu na kumhakikishia kuwa yeye ndiye Mkuu wa Mkoa wa Arusha; na hakuna mabadiliko yoyote kwa sasa, labda afikirie kumpandisha cheo zaidi; na sio kumuengua katika nafasi hiyo.
Mkuu huyo alisema baada ya kuzungumza kwa simu na Rais, Rais aliomba kuongea na kiongozi wa chama cha wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha na akamkabidhi simu Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Arusha, Wolter Maeda.
Maeda alikiri kuongea na Rais Magufuli na kusema kuwa Rais amemwambia kuwa Arusha, inatakiwa kuwa ya amani na utulivu na aliwaasa kufanya biashara bila ya wasiwasi na kulipa kodi inayostahili.
Source: mtembezi
0 comments:
Post a Comment