Tuesday, October 18, 2016

JK, Lowassa ana kwa ana msibani Dar

Jakaya Kikwete na Edward Lowassa walikuwa marafiki na sasa ni maadui wakubwa wa kisiasa, lakini jana walilazimika kushikana mikono wakati wa ibada ya kuaga mwili wa kada wa CCM, Didas Masaburi.


Mbali na tukio hilo, Rais John Magufuli alituliza wafiwa alipoeleza kuwa Masaburi, ambaye alizikwa jana chuoni kwake Chanika Dar es Salaam, ameacha wake wapatao watano na watoto zaidi ya 20 baada ya minong’ono kuibuka kutokana na aliyesoma wasifu kusema kada huyo ameacha mke mmoja wa ndoa na wajane wawili.

Source: Mwananchi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video 




0 comments:

Post a Comment