Kama wewe ni mpenzi wa muziki mzuri naamini jina la Chinbees halitakuwa geni maskioni mwako.
Kwasababu ni chorus killer wa maana, na amesikika kwenye hits kama Arosto ya G-Nako, Sweet Mangi yaNikki wa Pili, Mwendokasi ya Quick Rocka na nyingine kibao.
Ukiachana na kushirikishwa, yeye pia anamiliki hits kama “Niko Mbali” na hata Zuzu. Na pia ni muandishi mzuri wa mashairi, melodies na vitu kama hivyo kiasi kwamba hata “Kamatia Chini” ya Navy Kenzoinasemekana kuwa uandishi wake umehusika humo ndani.
August 4 ndio siku ambayo ngoma ya Zuzu iliachiwa rasmi, na hadi sasa ngoma hiyo imefanikiwa kufanya poa kiasi chake na kuchangia kulisogeza jina la Chinbees katika Mainstream.
Sasa Perfect255 ikaona haitakuwa kesi kama ikimnyamata Chinbees na kumuuliza amejipanga vipi katika kazi zijazo baada ya ngoma Zuzu kukimbiza kitaani.
“Zuzu Video comming soon, imeshakamilika kila kitu, ni mipango tu ya hapa na pale ili iweze kuachiwa. Na pia kuna ngoma nyingine ambayo inaitwa Ruba, nayo ipo Audio & Video lakinin itaanza Audio kisha Video.”
0 comments:
Post a Comment