Kundi la kigaidi la Al-Shabab kwa mara nyingine limeingia nchini Kenya na kufanya mashambulizi kadhaa ambayo yanadaiwa kuangamiza watu kadhaa na kujeruhi wengine.
Wanamgambo hao walivamia mji wa Mandera ambao wakazi wake wengi hutokea maeneo tofauti tofauti na mji huo na kufanya mashambulizi ya mabomu kabla ya kufyatuliana risasi na wana usalama wa serikali ya Kenya.
Maafisa polisi wa Kenya wamedai watu wanne wamethibitishwa kufariki na wengine wanne wakijeruhiwa kutokana na shambulio hilo. Hii si mara ya kwanza kwa wanamgambo wa Al-Shabab kuushambulia mji wa Mandera. Na hii inatokana na ukaribu uliopo baina ya mji huo na nchi ya Somalia linapotokea kundi hili la kigaidi la Al-Shabab.
Kwa muda mrefu sasa wanamgambo wa Al-Shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi kwa serikali ya Somalia inayoungwa mkono na umoja wa mataifa.
Source: mtembezi
0 comments:
Post a Comment