Sunday, September 25, 2016

MILIONI 187 ZAPATIKANA KATIKA MCHEZO WA WABUNGE MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA, AMBAO WABUNGE WA YANGA WAMESHINDA 5- 2 SIMBA


Jumla ya shilingi milioni 187 zimepatikana kupitia mchezo wa kirafiki baina ya Wabunge Mashabiki wa Yanga na Simba kwa ajili ya kuwachangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Mchezo huo ambao ulichezewa leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga wametoka kifua mbele kwa kufunga mabao matano kwa mbili. Yanga 5-2 Simba


Akizungumza Waziri Mkuu Majaliwa mara baada ya kumalizika kwa mpambano huo, aliwashukuru wabunge na watu wote waliojitokeza kuiunga mkono kampeni hiyo iliweza kuleta matunda hayo.Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. 
William Ngeleja ambaye ni shabiki wa timu ya Simba akizungumza mara baada ya mechi kumalizika.Waziri Mkuu Majaliwa akiwakabidhi kombe mashabiki wa timu ya Yanga ambao waliweza kushinda kwa bao 5-2.Waziri Mkuu Majaliwa akiwagawia Medali.


Shangwe na vigeregere vilitawala uwanjani hapo.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndungai akitoa shukrani kwa wabunge na ndugu, jamaa na marafiki walioweza kujitokeza

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndungai akitoa shukrani kwa wabunge na ndugu, jamaa na marafiki walioweza kujitokeza.

0 comments:

Post a Comment