Friday, June 23, 2017

Nimefurahi kukutana nawe Ebitoke” – Ben Pol

kupitia Instagram yake Ben Pol ameweka picha akiwa na Ebitoke na kuweka maneno ambayo yanaelezea hisia zake pia kwa kilichofanywa na mchekeshaji huyo kwa kuheshimu hisia zake.
“Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika?
“Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, labda huyo Mtu kesho hatokuwepo.
“Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SANA maishani, najua wengi walikubeza sana , wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na Mimi.. lakini huwezi amini Mimi nimefurahi mno!! kukutana na wewe na kuongea, na nimepata jambo kubwa sana. Na Nitayaishi Maneno yako 🙏🏽😍. Nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie. You are THE BEST 💪🏾!!@ebitoke #blessed🙏🏽” – Ben Pol.


Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment