Friday, June 23, 2017

Lioneil Messi na baba yake wafanikiwa kuikwepa jela

Almanusra mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lioneil Messi na baba yake waende jela baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya ukwepaji kulipa kodi.
Mwezi July mwaka jana Lioneil Messi na baba yake walikutwa na hatia katika kesi hiyo iliyokuwa ikiwakabili na baada ya hukumu waliamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo.
Messi na baba yake walihukumiwa kifungo cha miaka 21 japokuwa kifungo hicho kilikuwa cha nje ya gereza kwa kuwa ilikuwa ni chini ya miaka miwili.
Messi na baba yake waliajiri kundi la mawakili ambao walijaribu kuwatete katika kesi hiyo bila mafanikio na baadae mamlaka za kisheria zikawahukumu.
Sasa taarifa zinasema Lioneil Messi amekubali kulipa faini ya euro 252,000 na baba yake akilipa euro 180,000 na hiyo itawafanya kuepuka kifungo kilichokuwa kinawakabili.
Huu ni muendelezo wa makosa ya ukwepaji kodi nchini Hispania ambapo Cristiano Ronaldo na kocha Jose Mourinho nao wapo katika uchunguzi wa kesi kama ya Messi na baba yake.

Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment