Thursday, November 17, 2016

MPEMBA ALIYETAJWA NA MAGUFULI AFIKISHWA MAHAKAMANI

Watu sita akiwamo Yusuf Ali Yusuf maarufu Shehe au Mpemba aliyetajwa na Rais John Magufuli na wenzake watano, jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwamo la kujihusisha na mtandao wa uhalifu na kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh785 milioni.

Washtakiwa wengine ni Charles Mrutu maarufu Mangi Mapikipiki au Mangi Mpare, Benedict Kungwa, Jumanne Chima maarufu Jizzo au JK, Ahmed Nyagongo na Pius Kulagwa.



Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video






0 comments:

Post a Comment