Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani na Maafisa wa Polisi nchini Kenya baada ya kumshambulia kwa kisu Afisa Mmoja wa Polisi aliyekuwa akilinda usalama eneo la Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.
Kutokana na tukio hilo Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umelazimika kufunga shughuli zake zote siku ya leo ili kupisha uchunguzi zaidi. Maafisa wa usalama wa Kenya wakishirikiana na maafisa wa Shirika la Kijasusi la Marekani (FBI) wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.
Uchunguzi unaoendelea kuhusu tukio hilo una lengo la kubaini endapo mtu huyo ana washirika wengine ama la. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 24 alimvamia afisa usalama na kumdunga kisu hali iliyopelekea kupigwa risasi na kuuawa.
Hata hivyo maafisa wa ubalozi huo hawajadhurika na tukio hilo.
Source: mtembezi


0 comments:
Post a Comment