Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea masikitiko yake juu ya matumizi mabaya ya picha zake mitandaoni.
Kikwete ambaye alikuwa Rais wa awamu ya nne, kupitia ukurasa wake wa twitter amesema watu wamekuwa wakitumia picha hizo katika mambo yao yakisiasa.
“Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza malengo yao ya kisiasa,” aliandika twitter.
Aliongeza, “Nimestaafu naomba niachwe nipumzike. Nisingependwa kuhusishwa na siasa za mtandaoni dhidi ya Serikali. Namuunga mkono Rais na Serikali yake,”.
Source: bongo5


0 comments:
Post a Comment