Thursday, September 22, 2016

BAADA YA MAN U KUSHINDA GAME YA JANA EFL, YAPANGWA NA MAN CITY KATIKA HATUA INAYOFUATA

Baada ya kupokea vichapo vitatu mfululizo
ndani ya wiki moja klabu ya Manchester
United yenye kufundishwa na kocha mzoefu
Jose Mourinho hatimaye usiku wa jana wame washa mwanga katika mchezo wa kombe la
ligi.






Manchester United wameweza kupata ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Northampton katika uwanja wa ugenini wa klabu hiyo.
Ni mchezo ambao ulikuwa wa hatua ya tatu ya michuano hii ambapo Manchester United waliweza kupata ushindi kutoka kwa Michael Carrick, Ander Herrera na Marcus
Rashford.
Hivyo basi Man United imefuzu kuendelea
katika hatua ya nne na katika hatua hiyo
wamepangiwa kukutana na watani wao
klabu ya Manchester City,hii ni derby tena inajirudia katika kipindi kifupi baada ya ile iliyopigwa Septemba 10 na Man United kufungwa goli 2-1.

Pia ipo ratiba ya michezo yote ya hatua ya nne ya michuano hii ya EFL, hii hapa.
MICHEZO YA HATUA YA NNE EFL
•Manchester United V Manchester City
• Liverpool V Tottenham Hotspurs
• West Ham V Chelsea
• Arsenal V Reading
• Bristol City V Hull City
• Southampton V Sunderland
• Leeds United V Norwich
• Newcastle United V Preston
Michezo hii ya hatua ya nne itaanza kupigwa October 24 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment