Wednesday, July 12, 2017

Mapato ya serikali yafikia trilioni 14/-

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa yalikuwa Sh trilioni 14.4.
Makusanyo hayo yana ongezeko la asilimia 7.67 ya makusanyo yaliyofanywa na TRA katika mwaka wa fedha wa 2015/16 ambayo yalikuwa Sh trilioni 13.3. Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi, Richard Kayombo alisema kwa Juni ilikusanya kiasi cha Sh trilioni 1.37.

“Tunawashukuru wananchi wote ambao wametusaidia kukusanya kiasi hicho, kodi hizi ndizo zinazoiwezesha serikali kufanya shughuli zake za maendeleo,” alieleza Kayombo. Kayombo pia alisema mamlaka imeendelea kukusanya kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo na mwitikio wake umekuwa ni wa kiwango cha kuridhisha.
Alisema aliwashukuru wananchi wanaojitokeza katika ofisi mbalimbali za mamlaka nchi nzima ili kulipia kodi hiyo ya majengo ambayo mwisho wake wa kulipa ni Julai 15, mwaka huu.
“Zimebaki siku nne tu za kulipia kodi hii, tunawaomba wananchi wajitokeze kulipia kodi hiyo,” alisema na kuongeza kuwa TRA imeboresha huduma katika ofisi zake kuhakikisha wananchi hawakai muda mrefu kwenda kulipia kodi hiyo.
Aliongeza kuwa TRA inatoa mwito kwa wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki (EFDs) pindi wanapouza bidhaa au huduma na wananchi wote, kuhakikisha wanadai risiti pindi wanaponunua bidhaa au huduma

Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment