Ni siku iliyosubiriwa karibia na kila mpenzi wa soka duniani, siku ya kuamua kama Real Madrid watatetea kombe la Champions League au Juventus wataondoka nalo.
Massimiliano Allegri ameshatoa onyo kwa wapinzani wao na kuwaambia wazi kwamba leo haitakuwa rahisi kwani Juventus hawatakuwa na mchezo hata kidogo.
“Tutaingia kupambana, kwa mwaka mzima tulijipanga kuhusu hili na tunajua haitakuwa rahisi kucheza dhidi ya timu ambayo ni bingwa mtetezi”
“Makombe yote na ushindinwote tuliopata msimu huu vinatujenga zaidi kwenda kukabiliana na Real Madrid hii leo, ni mechi tunayopaswa kujiamini ili kuchukua kombe hili” alisema Alllegri.
Aliongeza kuwa “mwaka 2015 tuliongia kwenye fainali lakini nadhani hatukuwa imara sana na wala hatukujiamini lakini safari hii ni tofauti na hakika sisi ni bora”
Wakati Allegri akiongea hayo, kocha ambaye anapewa nafasi kuwa kocha wa kwanza kutetea kombe hilo Zinedine Zidane naye alikuwa na yake kuelekea mchezo huu wa leo.
“Msimu huu tumefanya kazi kubwa sana na kishinda kombe la La Liga na kufika katika fainali hii lakini kubwa sana kwetu ni kwa jinsi gani tumejiandaa kucheza katika fainali hii”
“Binafsi nimeshapoteza mechi nyingi na najua kama ilivyo kwa Juventus mmoja wetu anaweza kupoteza, cha muhimu ni kujitahidi kucheza mchezo wetu wa kila siku”
“Tunaweza kupewa nafasi katika mchezo huu lakini hii ni fainali na wote tuna nafasi ninkama tuko 50 50 lakini nategemea mchezo wa wazi kwa pande zote” alisema Zidane.
Vikosi vinaweza kuwa hivi Juventus, Buffon,Barzagli,Chiellini,Bonucci,Sandro,Khedira,Pjanic,Alves,Dyabala,Mandzukic,Higuain na Real Madrid wanaweza kupanga hivi Navas,Carvajal,Ramos,Varane,Marcelo,Modric,Casemiro,Kroos,Isco,Benzema,Ronaldo.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment