Manchester United wamefanikiwa kuingia katika fainali za mashindano ya Europa ambapo wanaenda kukutana na Ajax katika dimba la Friends Arena siku chache zijazo.
Kuna mambo mawili makubwa kwa United,moja wanaweza kufungwa mchezo huo na kupoteza nafasi ya kushiriki champions league msimu ujao au washinde mchezo huo na msimu ujao wawepo champions league.
Dua kubwa kwa mashabiki wa Manchester United ni washinde mchezo huo, kufungwa katika mchezo huo sio tu kwamba kunaweza kuwasononesha bali pia kutawaingiza katika hasara kifedha.
Imefahamika United wanaweza kuingia hasara ya kiasi cha pesa cha kuanzia £40m hadi £50m endapo tu watakubali kipigo katika fainali hiyo ya Europa.
Kwanza wadhamini wa Manchester United kampuni ya vifaa vya michezo Adidas itawabidi kuchomoa kiasi kadhaa katika £750m wanayoipa Manchester United ikiwa ni sehemu ya dilu lao la miaka 10.
Adidas wataikata United kiasi cha £20m ikiwa ni sehemu ya makubaliano yao endapo timu hiyo ikishindwa kushiriki katika Champuons League kwa mara ya pili.
Lakini sii hivyo tu bali pia United watapoteza kiasi cha £30m kiasi ambacho klabu hiyo hupewa kila mwaka kutokana na masuala ya matangazo ya luninga endapo wakifanikiwa kushiriki michuano ya champions league.
source:shaffihdauda
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment